Pin Song

Joh Makini aeleza kwanini Davido ana mzuka zaidi na kobalo ya wimbo wao mpya

Joh Makini aeleza kwanini Davido ana mzuka zaidi na kobalo ya wimbo wao mpya

Msanii wa muziki wa hip hop, Joh Makini amefunguka kwa kueleza sababu ya Davido kuwa na mzuka na kalabo ya wimbo wao mpya.
kiongea na Bongo5 wiki hii, Joh Makini amedai labda Davido ana mzuka na kalabo hiyo kwa kuwa yeye ndiye aliyeitafuta.

“Mimi naona ni kwasasabu alikuwa excited sana kufanya kazi na mimi, halafu wakati wa kufanya hii ngoma yeye ndiye aliyekuwa wakwanza kuniapproach mimi. Kwa hiyo nafikiri ni mtu ambaye alinifuatilia na akaupenda muziki wangu ndiyo maana hata chemistry imekuwa nzuri na tumefanya kitu kikubwa,” alisema Joh Makini.

Rappa huyo alisema tayari wameshashoot video ya wimbo wao mpya na muda wowote wataichia.