Pin Song

MOI waanza kutumia mfumo huu katika utoaji matibabu

MOI waanza kutumia mfumo huu katika utoaji matibabu

Taasisi ya Mifupa Muhimbili MOI imeanza kutumia mfumo wa kielektroniki katika utoaji wa matibabu hatua ambayo imesaidia kupunguza foleni na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma.
Mtaalam wa Takwimu katika Taasisi hiyo , Daniel Mulokoko amezungumza hayo, hospitali hapo ambapo amesema kuwa mfumo huo utasaidia kuangalia taarifa zao.

“Hii mitambo tunaweza tukafanya vitu vikaenda haraka I mean TEHAMA kama unavyojua kwahiyo vitu vinaenda haraka na hata ukija kuangalia sisi tukaipa mwendokasi kwa maana inafanya vitu haraka haraka tofauti na kuanza kutumia tena ni touch screen kama unavyoona inamuelekeza mtu process za mbele,” alisema Mulokoko.

Kwa upande wake, Afisa uhusiano MOI Patrick Mvungi amesema mfumo huo utawawezesha wagonjwa kupata taarifa zao hivyo kupunguza usumbufu kwao.