Pin Song

Griezmann hajafurahishwa na wenzake wa Ufaransa kumpongeza Varane kutwaa UEFA

Usiku wa June 6 moja kati ya video zilizokuwa zinasambaa katika mitandao ya kijamii ni kuhusiana na wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa pamoja na kocha wao Didier Deschamps kumpongeza Raphael Varane kwa kutwaa Champions League akiwa naReal Madrid.Varane ambaye alikuwa pamoja na wachezaji wenzake wa Ufaransa katika kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa alipongezwa na wachezaji wenzake wote pamoja na viongozi wa benchi la ufundi kasoro mchezaji mwenzake Antoine Griezmann anayeichezeaAtletico Madrid hakuonekana kufurahishwa.Griezmann katika video hiyo fupi kaonekana katika vipande viwili tofauti cha kwanza kutokumpa mkono wa pongeza na cha pili hakupiga makofi wakati wenzake wote kwa pamoja walikuwa wanampongeza, Real Madrid ilimtoa Atletico Madrid katika nusu fainali ya Champions League hiyo intajwa kuwa sababu.
VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagerahttps://youtu.be/hQ5jx8q7df4