Pin Song

Jamal Malinzi amkwepa Diamond na Alikiba


Rais wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, Jamal Malinzi Ijumaa hii amewashukuru wote waliokuwa wakiisapoti Serengeti Boys huku akishindwa kuzizungumzia tetesi za Diamond na Alikiba kutoonyesha ushirikiano walioutarajia.
Alisema hayo baada ya kuulizwa na mwandishi kwamba wao kama TFF waliichukuliaje taarifa ya kwamba Diamond na Alikiba kukataa kuonyesha ushirikiano mbele ya kamati ya uhamasishaji iliyoongozwa na wajumbe 10.
Waimbaji hao wawili ambao ni washindani wakubwa katika muziki, walichaguliwa na aliyekuwa Waziri wa Habari, Nape Nnauye kuwa kwenye kamati ya kuhamasisha Watanzania kuchangia timu ya Serengeti Boy.
Akijibu swali hilo, Jamal Malinzi alisema, “Naomba nisiongee chochote kuhusu Diamond na Alikiba naomba sana, mimi nashukuru tu ni wenzetu walichaguliwa kuingia katika kamati ya uhamasishaji ya Serengeti Boys basi mimi niishie kuwashukuru tu”
Mmoja kati ya wajumbe wa kamati hiyo, Maulid Kitenge ambaye pia ni mtangazaji wa EFM alidai Diamond na Alikiba walishindwa kuonyesha ushirikiano mbele kamati hiyo.
Serengeti Boy ilitolewa katika mashindano ya AFCON U-17 kwa kanuni ya head to head na Niger.