Pin Song

KRC Genk ya Mbwana Samatta imepoteza nafasi ya Europa League

Usiku wa May 31 2017 Club ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta ilicheza game yake ya mwisho ya play off ya kuwania kushiriki michuano yaUEFA Europa League msimu wa 2017/18 dhidi ya KV Oostende.
KRC Genk ambao msimu uliyoisha walifanikiwa kushiriki michuano ya Europa Leaguena kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali na kutolewa na Celta Vigo ya Hispania, hata hivyo Genk wamejikuta wakikubali kipigo cha magoli 3-1 wakiwa ugenini dhidi yaKV Oostende.
Kama Genk wangefanikiwa kupata ushindi katika mchezo huo uliyochezwa katika uwanja wa Albertpark, wangekuwa wamepata nafasi ya kushiriki michuano ya Europa League kwa mara nyingine tena, magoli ya Joseph Akpala dakika ya 27, David Rozehnal dakika ya 32 na Andile Jali dakika ya 51 ndio yaliyoimaliza KRC Genk.
Mtanzania Mbwana Samatta ambaye alipata nafasi ya kuipigania timu yake kwa dakika zote 90, hakufanikiwa kufunga goli licha ya timu yao kuutawala mchezo kwa asilimia 54 kwa 46 dhidi ya wenyeji wao na waliishia kupata goli la kufutia machozi dakika ya 43 kupitia kwa Siebe Schrijvers.