Pin Song

Michezo ya nusu fainali kombe la dunia U-20 kupigwa leo


Mashindano ya kombe la dunia kwa vijana walio na umri chini ya miaka 20 yanaendelea hii leo huko Korea Kusini kwa kuzikutanisha timu ya taifa ya Urugua dhidi ya Venezuela katika hatua ya nusu fainali.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Uruguay wakishangilia baada ya kuingia hatua ya nusu fainali
Katika hatua ya robo fainali timu ya taifa ya vijana ya Uruguay walio watoa Ureno na hivyo kukutana na Venezuela walio waondosha Marekani katika hatua kama hiyo.Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Daejeon.
Mchezo wa pili wa nusu fainali utachezwa ni kati ya Italia dhidi ya Uingereza mchezo ambao utafanyika katika dimba la Jeonju.
Mchezo wa fainali unatarajiwa kuchezwa Juni 11 ya mwaka huu katika uwanja wa Suwon.