Pin Song

Promota amtabiria makubwa Klitschko kwenye marudiano na Jushua


Promota, Eddie Hearn  anaamini bondia,Wladimir Klitschko kama atakubali mchezo wa marudiano dhidi ya Anthony Joshua basi mchezo huo utakuwa mgumu kwani atakuwa ni mwenye kujiamini zaidi .
Bondia Anthony Joshua akizipiga dhidi ya Wladimir Klitschko Cardiff mwezi November
Joshua, ambaye alimpiga Klitschko katika uwanja wa Wembley mwezi Aprili, na Promota wake wameridhia kuchezwa  kwa mchezo huo wa marudiano baina ya mabondia hao wawili wa uzito wa juu lakini lakini ufanyike mwezi Desemba.
Bondia Anthony Joshua akizipiga dhidi ya Wladimir Klitschko Cardiff mwezi November
Itakuwa bonge la mchezo kwa sababu Anthony Joshua ataingia katika mchezo huku akiwa na kumbukumbu za kuumizwa katika mchezo uliopita wakati, Wladimir Klitschko pia akiwa na kumbukumbu za kupoteza mchezo ” Hearn ambaye ni promota wa ngumi aliuambia  mtandao wa Sky Sports News HQ.