Pin Song

Tetesi za usajili ligi kuu nchini Uingereza


Dili la klabu ya Manchester United, kumsajili mchezaji, Alvaro Morata wa klabu ya soka ya Real Madrid kwa dau la pound 52.4m lagonga mwamba.
Mchezaji wa Real Madrid,Alvaro Morata
Kwa mujibu wa mtandao wa Sky Sports News HQ, umeripoti kuwa Madrid imekataa dau ya paundi milioni 52.4 kutoka kwa Man United ambao walikuwa wanamtaka kumsajili mchezaji huyo. Katika ofa hiyo golikipa wa United, David de Gea hakuhusishwa katika dili hilo, wakati Madridi ilipohitaji paundi milioni 78.
Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Hispania ameshinda jumla ya magoli 20 katika mashindano yote ya msimu uliomalizika hivi karibuni ndani ya kikosi cha Real na kuifanikisha kutwaa kombe la La Liga pamoja na klabu bingwa barani Ulaya.
Inadaiwa kuwa kama United ya Uingereza itashindwa kumsajili Morata, basi itaelekeza nguvu zake kwa mchezaji wa Torino, Andrea Belotti kwa kutoa dau la Euro milioni 100 [pound 87.3m].
Nayo klabu ya Liverpool imeanza mazungumzo na kiungo wa Sporting Lisbon, Gelson Martins. Majogoo hao wa Anfield tayari wameshaanza mazungumzo na Lisbon kupata saini ya mchezaji huyo imeeleza chombo cha habari cha Sky Sports News HQ
Kiungo wa Sporting Lisbon, Gelson Martins
Meneja, Jurgen Klopp ameshaanza na chaguo la kinda huyo wa kireno mwenye umri wa miaka 22, Martins ambaye msimu huu amekuwa akifuatiliwa na timu nyingi za barani Ulaya.
Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp
Mkataba wa Martins unamruhusu kuuzwa kwa dau la paundi milioni 46.5 kwa timu yoyote inayomuhitaji lakini vyanzo vinasema kuwa klabu ya Sporting ingekuwa tayari kumuza hata kwa paundi milioni 40 lakini mkataba huo ndio umekuwa kikwazo.
Wakati huo huo timu ya Arsenal imethibitisha kumsajili, Sead Kolasinac kwa uamisho huru na kuingia kandarasi ya miaka mitano ya kukihudumia kikosi cha Mzee wenger akitokea Schalke 04 ya Ujerumani.
Mchezaji aliyesajiliwa na klabu ya Arsenal, Sead Kolasinac
Naye mshambuliaji wa klabu ya Everton, Romelu Lukaku amefikia makubaliano na timu yake mpya. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Belgium amesita kutangaza timu atakayo kwenda kuichezea msimu ujao ila amekiri kuwa inacheza ligi kuu nchini Uingereza – Mchezaji huyo amekiambia chombo cha habari cha Sky.
Mchezaji wa klabu ya Everton, Romelu Lukaku
BY HAMZA  FUMO