Pin Song

Yanga yatupwa nje SportPesa Super Cup

Wawakilishi pekee wa Tanzania waliobakia katika mashindano ya kombe la SportPesa Super Cup, Dar Young Africans (Yanga) imetupwa nje katika hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.
Wachezaji wa klabu ya Yanga SC
Yanga wametolewa katika kombe hilo na AFC Leopards ya Kenya kwa mikwaju ya penati 4-3.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa vuta ni kuvute kwa pande zote mbili kulisakama lango la mpinzani wake umemalizika dakika 90 bila ya timu yoyote kuchomoza na ushindi.
Wachezaji wa klabu ya Yanga SC wakicheza dhidi ya AFC Leopard
Sasa Leopards wanamsubiri mshindi kati ya Gor Mahia dhidi ya Nakuru katika mchezo wa fainali ambao utachezwa Jumapili hii katika uwanja wa Uhuru.